
Jamaa mmoja ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya
mawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika tamasha moja
la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu kujiepusha na
vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa.Speech
ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo;
"Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja
anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa ugonjwa
huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini.
Jitahidini sana kukaa bila kupiga.
Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na
wala si kupiga piga kwani hii
gharama yake ni kubwa.Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa,
basi hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi
vinapatikana kwa wingi na gharama yake si kubwa.
Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara
yanayoweza kupatikana
kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.
Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina hatari
kubwa mno. Pia unashauriwa kutopiga tigo kabisa kwani hii
inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.
Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna hamu
angalau ya kupibu, lakini hii nayo ni hatari, kwani mwenzako
akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua
kupiga kabisa.
Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu
zitamaliza chaji, hii si kweli.Hakikisha tu kwamba simcard
iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu zote na ndio
inaongoza mawasiliano yote.
Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.
Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double skrini.
Hizo ni mbwembwe tu.Kuna simu nyingi sana feki siku hizi
zinauzwa zimevishwa cover mpya,usidanganyike.
Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu
inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana
kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi kuliko ile yenye
subscribers wengi."
asanteni kwa
kunisikiliza...


3:51 AM
Edward Mwasakafyuka

1 comments:
kaka hiyo co hotuba bali dongo kwa wadada
Post a Comment